Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi Arusha waanza kutekeleza agizo la Lugola

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amesema wameanza kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kuacha “kurusha majini” barabarani ili kuwaondolea bughudha wasafiri.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa leo Jumanne Machi 19, 2019, Kamanda Shana amesema maagizo aliyoyatoa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola wakati wa kikao cha wafanyabiashara Februari 21, 2019 kuacha kurusha picha za magari yaliyozidisha mwendo kwa askari walio kituo cha mbele.

Waziri Lugola alisema kitendo cha polisi kujificha na kupiga picha hakikubaliki bali wawe maeneo ya wazi kwa lengo la kuwapa elimu madereva na si kuweka kipaumbele kuwatoza faini na kurusha majini.

“Maelekezo ya Serikali hayana mjadala kuwa yanatekelezwa ama hayatekelezwi, alichokisema waziri wetu ndio msimamo wa Serikali na utekelezaji ulishaanza hata kabla mimi sijaamishiwa kituo cha Arusha,” amesema Shana.

Kuhusu kukabiliana na uhalifu hasa wa dawa za kulevya, Kamanda Shana amesema wanaojihusisha na biashara hiyo haramu watafute kazi halali za kufanya na kwa nafasi yake hatavumilia kuona mkoa wa Arusha unaendelea na biashara za bangi, cocaine na mirungi.



Chanzo: mwananchi.co.tz