Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pinda ashauri uwekezaji zaidi Dodoma

10445 Pinda+pic TanzaniaWeb

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri Mkuu mstaafu,  Mizengo Pinda amesema ili kuongeza uwekezaji kwa muda mfupi katika maeneo ambayo bado hayana mafaniko makubwa jijini Dodoma ni vyema Serikali ikawa tayari kuzungumza na

wawekezaji na kuondoa vikwazo kwao.

 

Akizungumza leo Juni 30 katika Shule ya Kimataifa ya One Planet jijini hapa, Pinda amesema uungwaji mkono wa uamuzi wa Rais John Magufuli wa kuhamishia Serikali jijini hapa unapaswa kuendana na uwekezaji katika maeneo yasiyofanikiwa.

 

“Moja ya eneo naliona linahitaji uwekezaji mkubwa ni katika elimu. Ukienda Dar es Salaam pale watu walijitokeza sana kuwekeza katika elimu lakini yote ile kuisaidia kutoa mchango ambapo Serikali peke yake haiwezi kuhudumia kikamilifu,” amesema.

 

Pinda amesema ili kuvuta wawekezaji wengi ni vizuri Serikali hasa mkoa kuangalia uwekezaji wa sekta ya elimu na afya tofauti na uwekezaji katika maeneo mengine ikiwemo viwanda.

 

“Kwa sababu elimu ni huduma si biashara ni kama ilivyo kwenye sekta ya afya kwa hiyo tukiweka uwekezaji unafanana na ule wa viwanda itakuwa ni vigumu kukuza sekta hiyo na kuifanya huduma hiyo iimarike kwa muda

mfupi,” amesema.

 

Ameshauri Serikali kuwa tayari kuzungumza vizuri na wawekezaji kwa kuwatia moyo na kuondoa baadhi ya vitu ambavyo ni vikwazo badala ya kuwa ni Serikali ya kuongeza vikwazo.

 

“Ikiwa ni (Serikali) ya kuongeza vikwazo tutapata tabu sana. Lakini mimi ninaamini chini ya uongozi wa Rais wetu Magufuli ambaye ndiye anasukuma sana suala la uwekezaji Dodoma, hili jambo halitatupa tabu hata kidogo upande wa Serikali,” amesema.

 

Mkuu wa Dodoma, Dk Benilith Mahenge amesema katika mambo mengi ambayo amekuwa akiulizwa na watu wanaofika ofisini kwake hasa mabalozi ni ardhi, huduma za afya na uwepo wa shule za kimataifa.

 

“Nimeulizwa hili na balozi wa Marekani, Urusi karibu mabalozi wote wanaulizi. Alichokisema Waziri Mkuu mstaafu (Pinda) tunakiunga mkono na tumeshaanza kukitekeleza tumeandaa profile (wasifu) wa investiment opportunity (fursa za uwekezaji)  za uwekezaji katika mji wa Dodoma,” amesema.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz