Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paroko kizimbani kwa tuhuma za wizi

Operanews1671027992793 Paroko kizimbani kwa tuhuma za wizi

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paroko wa Parokia ya Haydom  jimbo la Mbulu mkoani Manyara Bartazari Margwe Sule (63) amefikishwa katika mahakama ya mkoa wa Manyara kwa tuhuma za kuiba zaidi ya shilingi milioni 20 kwenye akaunti ya kaka yake Dionice Margwe Sule ambaye inadaiwa kuwa ni mgonjwa wa kupoteza kumbukumbu.

Inaelezwa kwamba  fedha hizo anazotuhumiwa kuziiba zimetokana na mirathi ya shemeji yake.

Kesi hiyo namba 44 ya mwaka 2022 imesomwa  na hakimu Mariam Luselwa katika mahakama ya mkoa wa Manyara.

Kesi hiyo inawakabili washtakiwa wa tatu Paroko wa Parokia ya Hydom Mbulu Manyara Baltazari Margwe Sule pamoja na watumishi wawili wa benki ya NMB Cynthia Nyamtiga miaka 27 na Winftida Rwakilomba miaka 30 kwa pamoja wametajwa mahakamni hapo kuhusika na kesi hiyo.

Imeelezwa mahakamani hapo, Paroko Baltazari anakabililiwa na makosa mawili, kosa la kwanza wizi kinyume na kifungu namba 258 kifungu kidogo cha kwanza na kifungu namba 265 vya kanuni ya adhabu sura namba 16 marejeo kama ilivyofanyiwa marejeo ya 2022.

Washtakiwa wengine ni watumishi wawili wa benki ya NMB Cynthia Nyamtiga pamoja na Winfrida Rwakilomba, ambapo Hakimu Mariam Luswelwa ameiambia mahakama washtakiwa hao kwapamoja wanakabiliwa na kosa la  Kushindwa kuzuia utendekaji wa kosa kinyume na kifungu 383 na kifungu cha 35 vya kanuni ya adhabu sura 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2022.

Washtakiwa hao watatu Paroko Baltazari Sule, Winfrida Rwakilomba na Cynthia Nyamtiga kwapamoja  wamekana kutenda mashtaka yanayowakabili.

Washtakiwa wote watatu wapo nje kwa sharti la kuwa na mdhamini mmoja kwa kila mshtakiwa na bondi ya  milioni saba kwa kila mdhamini.

Shauri hilo limepangwa tena tarehe 21 mwezi huu kwaajili ya kusomewa hoja za awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live