Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Panya Kalowa’ watikisa Dodoma

Panya Panya Kalowa

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KUNDI la vijana wadogo maarufu kama ‘Panya Kalowa,’ limeibuka katika maeneo mbalimbli ya Jiji la Dodoma ambapo limekuwa likifanya matukio ya kihalifu na kutishia usalama wa wananchi na mali zao.

Mashuhuda wa matukio hayo, wanasema kundi hilo hujumuisha watoto wanaosoma kati ya darasa la tano hadi kidato cha kwanza ambao hutembea nyakati za usiku kwa makundi ya watu kati ya 12 hadi 19.

Akizungumzia hali hiyo, Mkazi wa Medeli, Dotto Kusulya, amesema katika vijana hao wengi ni wanafunzi wa sekondari ambao wamekuwa wakijificha katika vichaka kuvizia watu wanaopita kisha kuwapora.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri, ametoa wiki mbili katika mitaa yote ya Kata ya Dodoma Makulu kuanzisha polisi jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live