Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paka aandika barua kwa mwenye nyumba akidai fidia Sh 150,000 kwa kupigwa

Paka Barua Paka aandika barua kwa mwenye nyumba akidai fidia Sh 150,000 kwa kupigwa

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paka wa ajabu ameibuka na kuzua taharuki miongoni mwa wakazi wa Mji wa Tunduma Mkoani Songwe ambapo wananchi wa eneo hilo wanadai kuwa paka huyo amekuwa akiandika barua na kuziacha mlangoni kwa mama mwenye nyumba.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao wamekuwa na hofu kubwa, wamedai kuwa paka huyo amekuwa akiandika barua hizo na kuziacha kwenye mlango wa mwenye nyumba akidai alipwe fidia ya pesa kiasi cha Tsh 150,000 kutokana na kipigo alichopatiwa hivi karibuni katika nyumba hiyo.

Aidha, wananchi hao wameeleza kuwa, paka huyo ni mkubwa kuliko kawaida na amekuwa akionekana kwa macho, lakini wananchi wanaamini anayefanya kitendo hicho ni binadamu mwenzao ambaye ameamua kujifanya paka.

“Anaandika barua anakuja kuziacha kwenye nyumba hii anasema anadai laki moja na nusu kutokana na kipigo alichopewa hivi karibuni. Huyu analeta barua lakini mtu mwenyewe hatumuoni,” wamesema mashuhuda hao.

Tukio hilo la aina yake linahusishwa na masuala ya kishirikina ambapo mamlaka za Serikali katika eneo hilo bado zinaendelea kufuatilia ili kubaini anayewafanyia wananchi kitendo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live