Joseph Kariuki Wanjiku (43) aliyekuwa Padri wa Kanisa katoliki, Parokia ya Mtakatifu Paulo, Jimbo Kuu la Nairobi, ameripotiwa kufariki baada ya kupoteza fahamu katika hoteli moja kaunti ya Murang'a, alipokuwa amepumzika na Mwanamke wa miaka 32 anayetajwa kuwa mpenzi wake na mfanyakazi mwenzie Parokiani.
Taaarifa ya Polisi imedai kuwa wawili hao waliingia Hotelini siku ya Ijumaa (Julai 7 usiku) kwa mapumziko, na ilipofika Julai 8, Saa 8 usiku, Mwanamke huyo aliwaarifu wasimamizi wa hoteli hiyo kwamba Kariuki alikuwa akipata kizunguzungu na kupoteza fahamu, ambapo alifariki dunia kabla ya kufikishwa hospitali.
Taarifa zaidi zinadai kuwa Mwili wa Karuki ulikutwa ukiwa umefunikwa nusu na shuka la kitanda cha hoteli, huku povu jeupe likitoka mdomoni na puani.