Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Operesheni Nyakuwa Nyakuwa yapamba moto

32484 Pic+nyakua Tanzania Web Photo

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Operesheni ya kuwakamata madereva wa magari wanaokiuka sheria za usalama barabarani kuanzia jijini Dar es Salaam hadi Arusha imeshika kasi.

Operesheni hiyo iliyopewa jina la Nyakuwa Nyakuwa inaongozwa na mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Muslim .

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Desemba 19, 2018, Muslim amesema lengo la operesheni hiyo ni kuzuia matukio ya ajali kutika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

"Magari yanayokiuka sheria za usalama barabarani  tunayakamata na hadi sasa magari zaidi ya 50 tumekamata na operesheni hii tunaifanya usiku na mchana,” amesema.

Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga, Solomon Mwangamilo ametoa wito kwa madereva kufuata sheria kwani wanaokiuka hawatapita salama mkoa wa Tanga.



Chanzo: mwananchi.co.tz