Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onyo la RC Iringa kwa madereva wa bajaji na pikipiki

Bod2 RC Iringa atoa onyo kali kwa madereva bodaboda na bajaji

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa moa wa Iringa, Queen Sendiga amewaonya askari wanaomiliki bajaji na bodaboda na kuwataka kuwaelekeza madereva wanaoendesha bajaji zao kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani.

Sendiga ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Iringa ambapo amesema siku za hivi karibuni ameshuhudia askari wa usalama barabarani akinusurika kugongwa na dereva bajaji baada ya askari huyo kumsimamisha.

"Kwa macho yangu mawili, nimeshuhudia dereva wa bajaji akitaka kumgonga askari wa barabarani mara baada ya kusimamishwa na askari huyo, kwa kifupi askari hawana nguvu mbele ya bodaboda na bajaji hapa Iringa,

"Nataka askari wa mkoa huu waheshimike, na haya mambo yote yote yanakuja kwa kuwa askari wanamiliki vyombo hivi vya moto ndio maana hawa madereva hawa wanakuwa na dharau kwa 'trafic', sasa natoa onyo " Amesema RC huyo.

Amesema lengo ni kuwaadabisha madereva hao pamoja na kupunguza ajali za barabarani mkoani hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live