Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ongezeko la watu tishio ikolojia ya Ngorongoro

Mifugo Ngoro.jpeg Ongezeko la watu na mifugo linatajwa kua chanzo cha uharibifu wa ikolojia.

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ngorongoro inateketea au hali ni mbaya Ngorongoro ndivyo unaweza ukasema kutokana na sababu mbalimbali zinazoashiria kuharibiwa na hatimaye kupotezwa kwa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro hifadhi yenye sifa lukuki ndani na nje ya nchi.

Ongezeko katika hifadhi hiyo ambapo limeongezeka maradufu kutoka watu 8000 mwaka 1959 wakati wanahamishwa kutoka Serengeti hadi zaidi ya watu 110,000 linasababisha madhara makubwa yanayopelekea kupotea kwa uhifadhi na madhara makubwa kwa wakazi wenyeji.

Kituo cha wanahabari watetezi wa Rasilimali na Taarifa (Media centre for Information and Resources advocacy - MECIRA) kimesikitishwa na hali ya Maisha duni wanayoishi wakazi wa tarafa ya Ngorongroro iliyomo ndani ya hifadhi kutokana na uduni wa Maisha unaotokana na changamoto kadhaa kubwa ikiwa ni kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu ndani ya eneo hilo la hifadhi kunakosababisha kuongeza umasikini wa wakazi husika.

Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iloyosainiwa na mkurugenzi mwendeshaji wa kituo hicho Habibu Mchange, wamesema kuwa tatizo lililopo Ngorongoro haliathiri uhifadhi pekee bali pia hata Maisha ya wananchi wa eneo hilo wanaathirika kutokana na ongezeko kubwa la watu kuliko uwezo wa eneo kuwahudumia

Mchange amewataka wanaharakati wote wanaojitokeza kupaza sauti, kuhakikisha wanasimama kwenye ukweli ili kuwanusuru wakazi wa eneo hilo ambao kwa hakika usalama wao kiuchumi, kiafya, kielimu na kiusalama ni mdogo sana kutokana na wingi huo wa watu

‘’Utafiti wetu tulioufanya kwa wiki mbili tatu hizi, pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali, taarifa mbalimbali na mazungumzo baina yetu na wakazi wa eneo husika, tumebaini kuwa mambo mengi yanayosemwa na wanaharakati kadhaa vna kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari hayana ukweli na kwa kweli yanapotosha umma na wakazi wa eneo husika hayawapendezi’’. Inasema sehemu ya taarifa hiyo.

‘’Kwa kweli tumegundua mambo mengi sana, tumegundua namna watoto wadogo wa kimasai wanavyotumikishwa kazi ya ufugaji kutwa nzima bila kujali kama kuna kwenda shule, tumegundua namna maradhi ya milipuko yanavyowatesa wakazi hawa, tumegundua namna umasikini ilivyokithiri kiasi ha watu zaidi ya asilimia 50 kuwa katika hali kubwa ya umasikini licha ya kuwaona wamezungukwa na mifugo mingi’’. Ananukuliwa Mchange katika taarifa yake hiyo.

‘’Taarifa zinasema mwaka 1959 palikuwa na watu chini ya 8000 tu, emagine mwaka 2017 watu walifika elf 94, leo hii wanakadiriwa kufika watu laki moja na elfu kumi na kidogo, kwa ukuaji huu wa watu kuna kila sababu ya watu hawa kutafutiwa maeneo huru ya kuishi ili waweze kujiendeleza bila kuathiri uhifadhi na mazingira, mle hifadhini kwa sheria inayosimamia uhifadhi hawataweza kupata haki yao ya maendeleo endelevu hivyo watakuwa masikini tikatika jambo ambbalo linawekana kabisa kuepukwa kwa wao kuondoka’’. Anasema zaidi.

Mchange anasema kuwa hadi sasa taarifa za NBS zinaonyesha kuwa pamekuwepo na hali ya kudumaa kwa uchumi kunakotokana na kukosekana kwa ambapo zaidi ya kaya 5,000 kati ya kaya 22,000 (22%) zilizopo hifadhini humo hazina mifugo.

Tunajiandaa kutoa taarifa rasmi ya uchambuzi wa hali ilivyo, ilivyokuwa na itakavyokuwa hivi karibuni, lakini kwa sasa sisi kama MECIRA pamoja na kutishwa kwetu kwa kuathirika kwa hali ya uhifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro, tunadiriki kusema kuwa hali pia ya Maisha ya wenyeji na mbaya pengine kuzidi maeneo mengi hapa nchini, na ubaya huu unatokana na kuongezeka kwao kwa kasi kubwa.

Taarifa zaidi zilizozifikia gazeti hili zinaonyesha kuwa miaka kadhaa nyuma zilihamishwa kwa hiyari zaidi ya kaya 110 kutoka hifadhini kwenda Kijiji cha JEMA kilichopo wilayani humo.

Hivi karibuni iliripotiwa kuwa Hifadhi ya Ngorongoro ipo hatarini kupotea na kupoteza uhai na umashughuli wake kutokana nna kukithiri kwa shughuli za kibinaadamu ikiwemo ufugaji uliopitiliza kiasi, ujenzi wa nyumba zisizofuata taratibu za kihifadhi na shughuli nyingine za kibiashara.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia makundi makubwa ya mifugo ikiwemo Ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, kuku, na mingineyo ikichukua eneo kubwa kuliko Wanyama wa asili wanaopendwa kufuatiliwa na watalii.

Pamoja na kuzingatia ukweli kuwa Ngorongoro ni hifadhi ni hifadhi ya kipekee inayowahusisha Wanyama binaadamu na mifugo kwa pamoja lakini hali ilivyo kwa sasa inatisha kiasi cha kutishia usalama wa hifadhi na wananchi husika wa asili wanaoishi katika eneo hilo.

Taarifa za uhakika ambazo zimepatikana ni kuwa mwaka 1959 wakati wakazi walioruhusiwa kuishi katika hifadhi hiyo kwa mchanganyiko wao na Wanyama pori, wakazi hao hawakuzidi watu elfu 9 tofauti na sasa wakazi hao wamefika zaidi ya laki moja na mifugo yao wanayoimiliki ikikadiriwa kuwa zaidi ya laki6.

‘’Kwa mujibu wa taarifa wanasema kuna mifugo laki 2 na nusu, nadiriki kusema sio kweli, mifugo hii haipungui haipungui laki saba hadi laki nane…hebu angalia tangu tumeanza kuanza makundi ya ng’ombe, mbuzi na kondoo sasa hivi ni zaidi ya masaa mawili tunazunguka tunawaona tu…hii maana yake kuwa hata kama watu hawa wapo kisheria lakini inahitajika jitihada za makusudi kunusuru tatizo hili…hili ni tatizo kwa kweli’’. Alisema Paul Schenzern Raia wa ujerumani aliyekuwa katika safari za kitalii.

Schezern ameongeza kuwa kwao wanavyoifahamu Ngorongoro nin kuwa eneo bora zaidi la kiutalii na kamwe hakuwaza kama angepita barabani akipishana na ng’ombe na mifugo mingine japokuwa alikuwa anaufahamu kuwa Ngorongoro wanaishi binaadamu na Wanyama lakini si kwa kiwango alichokiona.

‘’Nimetembea hifadhi kadhaa Duniani ambazo Wanyama na binaadamu wanaishi kwa asili, kwa kweli zinavutia n ahata kuishi kwao kunaemndana na uhifadhi wa mazingira, tofauti na hapa Ngorongoro…ntapata shida san akumshawishi mtu atakayeniomba ushauri juu ya kutaka kuja hapa. Nafikiri watetezi wa haki za binaadamu, mifugo, Wanyama na mazingira wanapaswa kupaza sauti ya pamoja kuinusuru hifadhi hii muhimu na bora’’. ameongeza.

‘’Unajua watu wanaweza kulalamika kwamba wanaishi humu na haipaswi kupangwa vizuri, lakini sio sahihi watetezi makini wa binaadamu wanatakiwa watetee kwanza usalama wa mazingira, usalama wa mazingira ya Ngorongoro ndio usalama wa Arusha, usalama wa Arusha ndio usalama wa Tanzania na ndio maana Dunia nzima kunakuwa na sheria kali zinazolinda mazingira...kujazana kwa watu na mifugo hifadhini sio haifai tu kwa mifugo bali haifai zaidi kwa binaadamu wanaoishi humo kwani kuishi kwao kunategemea zaidi ikolojia nya hifadhi husika’’. Alisema Habibu Mchange, Mratibu wa mtandao wa wanahabari wanarasilimali asilia na taarifa alipoombwa kutoa maoni yake.

Mchange amesema hata yeye alikuwa Ngorongoro mwishoni mwa mwaka jana na ameshuhudia ujenzi uliokithiri na unaovunja kabisa sheria na kanuni za uhifadhi na kuongeza kuwa anaandaa ziara ya wanahabari wanarasilimali asilia na taarifa kwenda kujionea hali ilivyo na kuuhabarisha umma na kuwataka wanaharakati kushirikiana kuokoa kivutio hicho muhimu.

‘’Hata mimi nilitembbea tembea mwishoni mwa mwaka, niliyoyaona Ngorongoro kwa kweli yanatisha na hayafai kusimuliwa hata kidogo, wadau nwa utalii, uhiofadhi na mazingira tusipochukua hatua na kupaza sauti, Ngorongoro itapotea kama upepo…..kwa kifupi tu nikuambie ndugu mwandishi kuwa NGORONGORO IPO HATARINI KUPOTEA’’. Ameongeza Mratibu Mchange.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live