Mon, 8 May 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo amebainisha kuwa tathimini inaonyesha dhana potofu ya kuua ndugu ili kupata mali (kafara) ni miongoni kiini kinachoshadadia matukio ya kikatili mkoani hapa.
Kamanda Jongo amebainisha hayo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kijiji cha Lwamugasa, kata ya Lwamugasa wilayani Geita na kueleza jeshi la polisi limejipanga kukomesha.
Amesema dhana potofu ya watu kuaminishwa kwamba wakiua ndugu zao watapata mali imewafanya watu kufanya ukatili kwa watoto na wazazi wao hali inayoendelea kuchafua taswira ya mkoa wa Geita.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live