Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Olenasha azishukia halmashauri 100 zilizopewa fedha za ujenzi wa ofisi

69061 Pic+olenasha

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Naibu Waziri wa Elimu nchini Tanzania, William Olenasha amezitaka halmashauri  100 nchini zilizopewa fedha za ujenzi wa ofisi za wadhibiti ubora wa elimu kukamilisha kwa wakati na kuzingatia ubora.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Julai 31, 2019 katika ukaguzi wa ofisi ya wadhibiti ubora wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara.

Amesema wataalam watafanya ukaguzi ili kuona thamani ya fedha iliyotolewa kama inalingana na  kazi zilizofanyika.

Mkuu wa Wilaya hiyo,  Nurdin Babu amesema mbali na ofisi hiyo wanaiomba wizara ya elimu kuendelea kusaidia  wilaya hasa ujenzi wa mabweni kwa shule za sekondari ili kuwawezesha watoto kusoma kwa urahisi.

Mdhibiti ubora wa elimu wilayani humo,  Nyoyo Andrew amesema ujenzi huo ulianza Julai, 2019 na kutarajiwa kukamilika Septemba 2019 kwa gharama ya zaidi ya Sh132 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz