Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa tarafa Simanjiro awatuliza wananchi nyongeza mishahara

54987 Pic+msha

Wed, 1 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mirerani. Watumishi wa Serikali nchini wametakiwa kuwa na matumaini na wasihofu kuhusu kupandishwa madaraja na mishahara, kwani Rais John Magufuli anaweza kufanya hayo leo jijini Mbeya.

Rai imetolewa leo Jumatano Mei Mosi na ofisa tarafa ya Moipo wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Joseph Mtataiko katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani.

Amewataka wafanyakazi wawe na matumaini ya kupandishwa mishahara kwani Rais Magufuli atatangaza neema hiyo kwenye maadhimisho ya kitaifa yanayoendelea jijini Mbeya.

Amesema kwa sababu miradi mikubwa ya kimkakati imefanikiwa na watumishi hewa wameshaondolewa wana uhakika leo watumishi wataongezewa mishahara mipya.

"Tusiwe na wasiwasi Rais Magufuli atasema neno na sisi tutapona kwani ni muda mrefu mishahara haijapandishwa kwa watumishi wa Serikali," amesema Mtataiko.

Naye ofisa mtendaji kata ya Endiamtu, Charles Msangya amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya wafanyakazi kwa mwaka huu ni uchumi wa kati inawezekana wakati wa mishahara bora kwa wafanyakazi ni sasa.

Related Content

Msangya amesema baada ya maandamano ya wafanyakazi na hotuba kutafanyika michezo mbalimbali ya kuadhimisha siku hiyo ikiwamo mchezo wa soka kati ya watumishi wa Serikali na madereva wa pikipiki maarufu bidaboda, kuvuta kamba, kukimbia na gunia na kukimbiza kuku.

Kwa uapnde wake, ofisa mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani, Evence Mbogo amesema maadhimisho hayo yanahusisha taasisi mbalimbali za Serikali na za binafsi.



Chanzo: mwananchi.co.tz