Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa Mifugo Makete apiga marufuku kuchinja, kula kitimoto

Pig 1000p Ofisa Mifugo Makete apiga marufuku kuchinja, kula kitimoto

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Mifugo na Uvuvi Wilayani Makete mkoani njombe, Aldo Mwapinga amepiga marufuku kuchinja au kula nguruwe kutokana na uwepo wa taarifa za vifo vya nguruwe 21 waliodaiwa kuwa na dalili za homa.

"Kata ya Tandala kumeripotiwa dalili za ugonjwa wa homa ya nguruwe kwa hiyo tunaendelea na jitihada za kuhakikisha tunashirikiana na watendaji kuanzia ngazi ya kata hadi vitongoji kutoa taarifa juu ya hali inavyoendelea," alisema.

Alisema: "Baada ya kupata taarifa hizi tumesimamisha zoezi la uchinjaji wa nguruwe katika kila eneo la kata ya Tandala, na pili kutoa nguruwe kuwapeleka kwenye maeneo mengine, pia tumezuia utoaji nguruwe kutoa zizi moja kwenda jengine kwa ajili ya kupandisha kwa jike," alisema Mwapinga.

Mwapinga, aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano pamoja na kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na wataalamu wa mifugo ikiwamo kuacha kufukua nguruwe waliofukiwa baada ya kufa, kuwachinja na kwenda kuuza nyama hizo vilabuni nyakati za usiku.

"Nawaomba wananchi watupe ushirikiano kwa kutupa taarifa kila kifo kinachotokea, kuacha kufukua mizoga ili kuhakikisha jamii yetu inakua salama kwa kufuata maelekezo," alisema Mwapinga.

Alisema, inawezekana kuutokomeza ugonjwa wa homa ya nguruwe na kuwa historia katika maeneo yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live