Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba yateketea mchana kweupe

Nyumba Motoz.jpeg Nyumba ikiteketea

Sun, 10 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia ya mzee Batista Mtewele wa Kihesa Njombe imenusuruka kupoteza uhai wao baada ya moto kuzuka katika nyumba yao ambao unadaiwa kuwa Chanzo cheke ni Shoti ya Umeme.

Mmiliki wa Nyumba hiyo mzee Batisha Mtewele ameeleza kuwa alipigiwa simu wakati akiwa kazini kwamba moto umezuka kwenye nyumba yake na ndipo kwa haraka alichukua hatua ya kurudi nyumbani ili kujua kinachojiri, ambapo mara baada ya kufika nyumbani hapo alikuta moto huo ukiwa tayari umeshazimwa kwa juhudi kubwa zilizofanywa na majirani zake.

Aidha, Mzee Batista amewashukuru sana majirani zake kwa jitihada na ushirikiano wao katika kuzima moto huo, lakini pia ameishukuru serikali kwa ushirikiano wake katika kukabiliana na majanga kama hayo hapa nchini.

#TanzaniaWeb.com

Chanzo: www.tanzaniaweb.live