Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba kuuzwa kisa deni la mahari

MAHAKA HI 1 Law Nyumba kuuzwa kisa deni la mahari

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyo ya kawaida, nyumba ya Seleman Mussa (65), Mkazi wa Kijiji cha Nkoma, wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu, iko hatiani kuuzwa kama fidia ya deni la Sh1.1 milioni, analodaiwa baada ya kutokamilisha kulipa mahari ya kijana wake.

Kijana wake huyo ambaye ni mwalimu wa shule moja ya sekondari mkoani Shinyanga, alimuoa binti wa Mwita Kati, toka mwaka 2019 kwa ndoa ya kimila, kwa makubaliano ya mahari ya ng'ombe 15.

Akizungumza nasi, Mussa amekiri juu ya makubaliano hayo kwa kusema: “Tulikubaliana mahari ya ng'ombe 15 kwa thamani ya Sh150, 000 kila mmoja, baada ya maridhiano, walikuja nyumbani wakasema wanataka mahari yote, lakini tuliwaomba wachukue nusu na inayobaki tutailipa baadae," amesema Seleman.

Hata hivyo kwa mujibu wa Seleman, ilipofika mwaka 2020 baba mzazi wa binti alianza kudai mahari iliyosalia, ndipo alipoomba muda wa kuendelea kutafuta pesa ili kukamilisha deni hilo, na hapo ndipo ugomvi ulipoanzia.

Baada ya vikao kadhaa vya kifamilia na kiserikali kushindwa kufikia muafaka, mdai alilifikisha suala hilo mahakamani ambapo hukumu ilitolewa.

Katika shauri hilo la madai namba 81 la mwaka 2020, hukumu ilitolewa ilitaka kukamata nyumba ya Seleman namba 27B iliyopo kijiji cha Nkoma ili kufidia kiasi cha Sh1.21 kilichokuwa kimebaki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live