Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba 556 zaathirika kwa mvua Geita, Serikali yatoa msaada

Burundi: Watoto 4 Wafariki Baada Ya Kanisa Kuporomoka Kufuatia Mvua Kubwa Nyumba 556 zaathirika kwa mvua Geita, Serikali yatoa msaada

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takribani nyumba 556 za makazi ya watu katika tarafa ya Kasamwa ndani ya halmashauri ya Mji wa Geita zimepata madhara kufuatia mvua zilizonyesha zikiambatana na upepo kuanzia Oktoba 18, 2023 hadi Novemba 10, 2023.

Mratibu wa maafa wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Valeria Makonda ameeleza hayo katika hafla ya ugawaji wa msaada kwa waathirika wa mafuriko ndani ya halmashauri hiyo.

Amesema Mkoa wa Geita tayari umepokea tani 22.1 za mahindi pamoja na vifaa vya msaada wa kibinadamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kaya ambazo makazi yao yaliharibiwa na mvua ikiwemo za halmashauri ya Mji wa Geita.

Valeria amebainisha miongoni mwa wanufaika wa msaada wa mahindi hayo ni waathirika wa nyumba hizo za makazi zilizoharibiwa na mvua, ambapo waathirika wamepatiwa msaada wa vyakula na malazi vilivyotolewa na serikali.

Katika taarifa yake kwa Mkuu wa wilaya Mratibu huyo wa Maafa ameeleza kuwa mpaka sasa kiasi cha Sh milioni 225.46 kinahitajika ili kukarabati miundombinu ya taasisi za umma zilizoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe akizungumza baada ya kugawa vifaa vya kibinadamu, amewataka waathirika wa mvua hizo kutumia vyema misaada waliyopewa na serikali na kuwaelekeza watendaji kufuatilia misaada hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live