Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba 500 zasombwa na mafuriko Nachingwea

Mafuriko Yaua Watu Wapatao 10 Kusini Mwa Msumbiji Nyumba 500 zasombwa na mafuriko Nachingwea

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya nyumba 500 zimebomoka kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha katika Kata ya Mbondo na Kilimarondo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.

Akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Nachingwea, Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo amesema kamati ya Maafa inafanya tathimini ya Maafa yaliyosababishwa na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kuwapa pole wahanga hao.

Moyo amesema Kata ya Kilimarondo ina jumla nyumba 326 ambapo nyumba 223 zimeanguka kabisa kutokana na Mvua.

Katika kata ya Mbondo jumla ya Kaya 290 zimebomolewa nyumba zao na kusababisha jumla ya wakazi 836 kukosa Makazi na kupoteza mali zao nyingi. Maafa hayo yametokea katika vijiji vya kata hiyo kama ifuatavyo katika kijiji cha Chimbendenga kaya 67, Mbondo kaya 149, Nakalonji kaya 36 na kijiji cha Naimba kaya 38.

Moyo alisema kuwa kwa upande wa Kilimo, Mashamba mengi yameathiriwa kwa kujaa maji na hali hiyo imepelekea mazao kudumaa na kubadili rangi kabisa Kitu kitakachosababisha uzalishaji kupungua kwa kasi kubwa kwa mwaka huu (2024) na mazao hayo ni Mahindi, mihogo, mtama na kunde.

Mvua imeharibu takribani heka 2245 kwa Kata ya Kilimarondo. Pia, miundombinu imeharibiwa, barabara zinazounganisha kijiji na kijiji hazipitiki na kufanya baadhi ya shughuli za uzalishaji kusiamama au kupungua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live