Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba 50 zabomolewa Dodoma kupisha ujenzi wa barabara

12281 BARABARA+PIC TanzaniaWeb

Thu, 16 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Nyumba zaidi ya 50 katika kata ya Nkhungu Halmashauri ya Jiji la Dodoma zimebomolewa kupisha ujenzi wa barabara.

Akizungumza leo Alhamisi Agosti 16,  2018 mhandisi wa Jiji hilo, Ally Bella amesema kuwa nyumba zaidi ya 200 ziliwekewa alama za x zaidi ya miezi miwili iliyopita.

“Hadi sasa hatuna idadi kamili ya watu wanaotakiwa kubomoa kwa sababu hata baada ya kupewa notisi bado waliendelea kujenga. Tukimaliza tutakuwa na idadi kamili," amesema.

Amesema wameweka alama hizo katika nyumba zaidi ya 200 katika maeneo mbalimbali ya kuanzia Shule ya Martin Luther hadi barabara ya Singida.

Hata hivyo,  amesema ni maeneo machache ambayo yana nyumba na kwamba mengi yana vibanda.

Mmoja wa waathirika wa ubomoaji huo,  Salima Kalosi amesema hawapingi kuondolewa katika maeneo hayo kwa sababu shughuli inayofanyika ni ya ujenzi wa barabara kwa ajili ya maendeleo, kwamba wanacholalamikia ni kutopewa taarifa.

“Nilikuwa na tofali 3,000 nilizitengeneza na kuziweka hapa ili zinisaidie huko ninakokwenda lakini wamezivunja zote,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz