Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba 339 zajengwa kwa waliopisha ujenzi bomba la mafuta

Bomba La Mafuta TANGA Nyumba 339 zajengwa kwa waliopisha ujenzi bomba la mafuta

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya nyumba 339 zimejengwa kwa ajili ya makazi ya kudumu kwa wanufaika waliopisha maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi nchini.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Mkoa wa Tanga, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Maulid Surumbu wakati wa hafla ya uhitimishaji wa tukio la ujenzi wa nyumba za makazi mbadala kwa walioguswa kupisha mradi bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki.

Amesema kwa Mkoa wa Tanga pekee mradi umejenga nyumba za makazi mbadala 43 kwa ajili ya wananchi 40 waliopoteza makazi kwenye maeneo mbalimbali ya mkuza ambayo yanapitiwa na mradi huo mkoa huo.

"Niwaombe wananchi muwe sehemu ya ulinzi wa miundombinu katika maeneo yenu ya mradi kwani mradi huu ni wa thamani sana, lakini una lengo la kuboresha uchumi wa nchi yetu,"amesema DC Surumbu.

Mratibu wa bomba la mafuta upande wa Tanzania , Asiad Mrutu amesema kuwa jumla ya walioguswa na mradi 9,822 kati ya 9,904 wamelipwa fidia ya zaidi ya sh Bil 34.9.mpaka Sasa.

Naye Mkurungenzi wa Utawala na Mawasiliano wa Mradi, Geoffrey Mponda, amesema kuwa mradi huo umezingatia sheria za nchi na taratibu za kimataifa katika ulipaji wa fidia ikiwemo kutwaa ardhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live