Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba 30 zaathirika kwa mvua

E166c7b98f46e74fd31215112c61982d Nyumba 30 zaathirika kwa mvua

Wed, 13 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

ZAIDI ya nyumba 30 zimeathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Bahi huku mbili zikibomoka.

Akizungumza na HabariLEO jana, Diwani wa Kata ya Bahi, Agustine Ndonu alisema nyumba zilizoathiriwa ni za vitongoji vya Madukani, Mnadani na Ngambo.

Alisema katika maeneo hayo zaidi ya nyumba 30 zilijaa maji huku mbili zikibomoka na kuwaacha wakazi wa nyumba hizo wakiwa hawana pa kulala.

Alizitaja kaya mbili zilizobomokewa na nyumba ni za Hassan Masudi na Yazidi Mrisho.

Alisema nyumba nyingi zilizoathiriwa ni zile zilizojengwa kwa tope.

Pia alisema ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaopita karibu na wananchi umekuwa ukisababisha baadhi ya maeneo kujaa maji kutokana na matuta waliyoweka wakati wa ujenzi na kusababisha maji kukosa njia ya kupita kwenye njia yake ya asili, hivyo kuathiri baadhi ya makazi ya wananchi.

Alisema tayari jitihada zinafanyika kwa ushirikiano wa wilaya, Shirika la Reli (TRC) ili kuhakikisha njia ya asili ya kupita maji inarejeshwa ili yasiathiri makazi ya watu.

Mmoja wa wananchi wa kitongoji cha madukani, Mussa Mganga alisema mvua za mwaka huu zimekuwa ni nyingi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari.

Chanzo: habarileo.co.tz