Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyumba 20 zaunganisha umeme bila utaratibu

D0c684004c409338b789a7ba58dc8b0a.jpeg Nyumba 20 zaunganisha umeme bila utaratibu

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAKAZI wa Mwanza wameonywa kuacha mara moja tabia ya kujiunganishia umeme kwani kufanya hivyo ni kinyume na Sheria.

Hayo yalisemwa na Mhandishi Mdhibiti wa Mapato katika Shirika la Umeme(TANESCO) mkoa wa Mwanza,

Rajab Marwa wakati wa ukaguzi wa kushitukiza katika maeneo mbalimbali mkoani hapa. Katika ukaguzi huo zaidi ya nyumba 20 zilibainika kujiunganishia umeme bila kufuata utaratibu.

Marwa alisema Shirika lao litaendelea kufanya ukaguzi huo mara kwa mara ili kubaini wabadhirifu wa miundombinu ya umeme.

“Wateja wa maeneo ya mlimani wana tabia

ya kujiunganishia sana umeme kutoka kwenye nguzo moja kwa moja jambo ambalo ni kinyume na sheria. Tunaomba wananchi wetu kuacha tabia ya kutumia vishoka,’’ alisema Marwa.

Alisema kwa upelelezi wa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza wamefanikiwa kukamata wahusika watatu waliojiunganishia umeme bila kufuata utaratibu na kuongeza

kuwa wananchi waache utaratibu wa kutumia umeme bila kufuata utaratibu uliowekwa na shirika lao.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mission, kata ya Pamba, Mussa Fereji alisema upelelezi na operasheni maalumu iliyofanywa na Tanesco pamoja na jeshi la polisi wamebaini katika mtaa wake kuna nyumba zaidi ya 20 zimejiunganisha umeme bila kufuata utaratibu maalumu.

Alisema atashirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha wanatoa elimu kuhusu umeme ili wakazi wa mtaani kwake waepuka tabia ya kujiunganishia umeme jambo ambalo ni hasara kubwa sana katika shirika la Tanesco.

Chanzo: www.habarileo.co.tz