Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyuki wajeruhi wanafunzi darasani

4f7c38cd18971a4de2a717b176418671 Nyuki wajeruhi wanafunzi darasani

Thu, 30 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANAFUNZI sita wa Shule ya Msingi Sanya Juu wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wamejeruhiwa baada ya kung'atwa na nyuki wakiwa darasani.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Beatrice Matella alisema, tukio hilo limetokea Julai 27 mwaka huu, saa 10 jioni wanafunzi wakiendelea na masomo.

Alisema, kundi kubwa la nyuki liliingia katika eneo la shule hadi madarasani na kusababisha wanafunzi kukimbia kunusuru maisha na wengine kung’atwa.

Matela alisema tukio hilo lilisababisha wanafunzi wanne wa darasa la nne na wawili wa darasa sita waumie na walikimbizwa hospitali ya wilaya.

Kabla ya kupelekwa hospitali wanafunzi walipata msaada kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilayani.

Wanachama hao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa ukumbi jirani na shule hiyo, wakipiga kura za maoni za kuchagua udiwani viti maalumu.

"Watu wa CCM walitusaidia, walileta magari kuwatoa walimu na wanafunzi katika eneo la shule na baadhi yao kupelekwa hospitali ya wilaya ili kupata matibabu na kuruhusiwa, ''alisema Matela.

Katika uchaguzi uliokuwa unasimamiwa na Katibu wa CCM wilaya, Mwanaidi Mbishi, wajumbe hao walipitisha majina saba ya walioongoza kura hizo.

Walioongoza ni Mjumbe wa Siha Magharibi, Christina Kavishe (167), Siha Mashariki Jane Kimaro ( 158), Siha Kaskazini, Tawida Basso (147), Siha Kusini, Lilian Molel ( 96), Siha Kati Egine Nzao (57), Sauda Lema (49) na Claudia Muro (44).

Chanzo: habarileo.co.tz