Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyang'hwale ina uhaba matundu ya vyoo 1,583, madarasa 608

Ccd5924b4379a0980f1b02ec1f5675d6 Nyang'hwale ina uhaba matundu ya vyoo 1,583, madarasa 608

Sat, 17 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Nyang'hwale, mkoani Geita, Jamhuri William amesema Halmashauri ya Nyang'hwale inakabiliwa na uhaba wamatundu ya vyoo 1,583 kwenye shule za msingi na sekondari hali inayohatarisha afya za walimu na wanafunzi.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo kwa Mkuu wa Mkoa Mkoa wa Geita, Rosemery Senyamule wiki iliyopita, Jamhuri alisema changamoto hiyo ya uhaba wa matundu ya vyoo inaenda sambamba na upungufu wa vyumba vya madarasa 556 kwa shule za msingi na madarasa 52 kwa shule za sekondari zilizo na vyumba 163 ingawa mahitaji ni vyumba vya madarasa 215.

Alisema wilaya hiyo yenye shule za msingi 69 zenye usajili na shule tatu zikiwa ni shikizi zina jumla ya wanafunzi 52,743, kati ya hao wasichana ni 27,078 na wavulana ni 25,665 pamoja na walimu 796 ambao wakiume ni 589 na wa kike 207.

Kwa upande wa shule za sekondari, alisema halmashauri hiyo ina shule 12 zenye jumla ya wanafunzi 8281, kati yao wavulana ni 5,990 na wasichana ni 2291, walimu wa masomo ya sanaa 186, walimu wa sayansi 78, huku kukiwa na upungufu wa walimu wa sanaa 14 na walimu wa sayansi 82.

Mkuu huyo wa wilaya alisema ili kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi, halmashauri hiyo imekamilisha ujenzi wa vyumba 35 na vingine 34 vipo hatua ya umaliziaji, hatua ya renta vyumba 69, hatua ya madirisha vyumba 12 na hatua ya msingi vyumba 35 na shule za msingi mpya saba zimejengwa.

Kwa shule za sekondari, alisema halmashauri hiyo inaendelea na ujenzi wa majengo 39 yaliyo katika hatua mbalimbali na majengo nane yapo katika ukamilishaji na imepokea walimu wa sayansi 12 mwaka huu na kupitia mapato ya ndani imetenga Sh milioni 70 kutengeneza meza na viti 1967 kwa ajili ya wanafunzi.

Baada ya kusikiliza taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Senyamule aliagiza ukamilishaji wa haraka wa majengo ya madarasa wilayani humo na kuahidi kuandaa kikao na wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri ili kuweka mikakati ya kumaliza uhaba wa madarasa zaidi ya 10,000 mkoa mzima.

Chanzo: www.habarileo.co.tz