Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyamisati wapatiwa kivuko

56448 Kivukonipic

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania imekamilisha zabuni ya ujenzi wa kivuko cha Nyamisati- Mafia na sasa wanashughulikia ununuzi wa injini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Isack Kamwelwe bungeni leo Alhamisi Mei 9, 2019 bungeni jijini Dodoma kwamba shughuli hiyo itakwenda sambamba na kivuko cha Ukerewe.

Kamwelwe amesema ujenzi wa vivuko hivyo ni muhimu kwa sababu wananchi wa maeneo hayo wanapata shida.

Waziri huyo alikuwa akijibu maswali ya nyongeza ya wabunge Ukerewe (CCM), Joseph Mkundi na Mbaraka Dau wa Mafia.

Katika swali la msingi mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku Musukuma ameuliza ni lini Serikali itajenga gati katika kijiji cha Izumacheli.

Mbunge huyo amesema meli inapaki juu ya jiwe jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria na chombo chenyewe.

Katika majibu yake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema Serikali inatambua tatizo hilo na kipaumbele kikiwekwa kwenye maeneo yenye mahitaji maalumu ikiwamo Geita eneo la Izumacheli.

Nditiye amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imeandaa programu ya namna bora ya uboreshaji wa huduma za usafiri katika Ziwa Victoria.



Chanzo: mwananchi.co.tz