Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyamagana Yajipanga tayari kwa uchaguzi

720138d195dc3f660390114554560074 Nyamagana Yajipanga tayari kwa uchaguzi

Tue, 27 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Kiomoni Kibamba amesema maandalizi yote yapo tayari kwajili ya uchaguzi mkuu unaofanyika kesho.

Akizungumza na Habarileo katika mahojiano malumu, Kibamba amesema maandalizi yalikamilika asubuhi ya jana. Amesema jumla jimbo hilo linawapiga kura 344,891 na vifaa vyote vimekamilika tayari. Alisema jumla kuna kata 18, vituo vya kupigia kura 895 na wasimamizi wa uchaguzi wapo 4475.

Amesema vifaa vya uchaguzi vimesindikizwa na maaskari pamoja na wasimamizi wasaidizi wa kata. Alisema anawaomba wapiga kura wawahi asubuhi na mapema kwajili ya upigaji kura.Alisema matokeo ya mgombea ubunge wa jimbo la Nyamagana yatatangazwa Alhamisi au Ijumaa ya wiki hii.

Chanzo: habarileo.co.tz