Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyama ya ng’ombe yapanda bei

NYAMA 1 Nyama ya ng’ombe yapanda bei

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bei ya nyama ya ng’ombe imepanda kutoka Sh6, 000 kwa kilo moja hadi Sh7, 000 kutokana na gharama za mfugo huo kuwa juu.

Akizungumza leo Jumanne Desemba 21, 2021 Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Nyama Sumbawanga, Francis Mwanyangala amesema bei ya nyama imepanda kwa sababu ya gharama za upatikanaji na uhitaji wa soko.

"Gharama za upatikanaji wa ng'ombe zimekuwa kubwa kuliko ilivyokuwa siku za nyuma ambapo walikuwa wakinunua ng'ombe wa kilo 120 kwa Sh450,000 lakini hivi sasa anauzwa kati Sh650,000 hadi 700,000" amesema Mwanyangala.

Amesema gharama za upatikanaji wa mifugo hiyo imesababishwa na wageni kununua ng'ombe, mbuzi na kondoo minadani ambapo ununua kwa bei ya juu hali inayofanya wafanyabiashara kukosa mifugo yenye ubora kwa ajili ya walaji wa mjini.

Hata hivyo baadhi ya wananchi hususani walaji wa nyama wameeleza masikitiko yao ya kitendo cha kupanda kwa bei ya nyama hiyo.

Mmoja wa watumiaji kitoweo hicho, Emiliana Godfrey amesema kitendo cha wauzaji wa nyama kupandisha bei ya nyama kwa kilo moja kutoka Sh6,000 hadi Sh7,000 msimu huu wa sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya hakikubaliki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live