Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Njombe yapatiwa Sh bilioni 277 miradi ya barabara

F1021b4aa7c1360c5d30175c2dabc04a Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali

Sun, 16 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkoa wa Njombe umepatiwa fedha Sh bilioni 277 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA).

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa leo Januari 16, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya Serikali ya miradi mbalimbali.

“Kuna miradi inayoendelea kutekelezwa bila kusimama, kama ujenzi wa barabara ya Njombe – Makete kilometa 107.4, ujenzi wa barabara nyingine ya Itoni – Ludewa – Manda (Km 211.42) kwa kiwango cha lami na zege, na ujenzi wa barabara za mjini,”amesema Msigwa.

Msigwa amesema upande wa afya Sh bilioni 7.2 zimepokelewa kwa ajili ya miradi mbalimbali katika kuimarisha sekta ya afya.

“Fedha hizi karibu zote zinapelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kuagiza dawa na vifaa tiba. Sasa tunataka mabilioni haya yaingie mifukoni mwa Watanzania,” ameongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live