Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Njaa yamtoa mafichoni mtuhumiwa mauaji ya mke wa mwenyekiti, akamatwa

Mke Wa Mwenyekiti Khadija Njaa yamtoa mafichoni mtuhumiwa mauaji ya mke wa mwenyekiti, akamatwa

Tue, 21 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paschal Kaigwa Mariseli (21) mkazi wa mtaa wa National housing kata ya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba anayetuhumiwa kwa mauaji ya Hadija Ismail (29) amekamatwa na jeshi la polisi mkoani Kagera baada ya kukaa mafichoni kwa siku sita.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na jeshi la polisi Jumapili Februari 19, 2023 baada ya kutoka mafichoni alikokuwa amejificha baada ya kuumwa njaa iliyomtoa kwenda kuomba msaada wa chakula nyumbani kwa shanghazi yake mtaa wa Kashai Katotorwansi manispaa ya Bukoba.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera, Wiliam Mwampaghale amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema kuwa wanaendelea kumuhoji mtuhumiwa ili jeshi hilo liweze kukamilisha upepelezi kwa ajili ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

“Mtuhumiwa wa mauji ya Hadija Ismail tumemkamata Februari 19,2023 majira ya saa 10:00 jioni baada ya kutekeleza mauji Februari 13,2023 na kwenda kujificha katika vichaka kwa muda wote huo na baada ya njaa kali aliamua kutoka mafichoni kwenda kwa shanghazi yake Kashai Katotorwansi kuomba chakula alipofika nyumbani shanghazi yake hakuwepo amewakuta watoto waliokuwa wanamfahamu ambao baada ya kumuona wamepiga kelele na majirani wamefika na kumkamata,” amesema Mwampaghale.

Ikumbukwe kuwa, kijana huyo anayetuhumiwa kwa mauaji alikuwa anaishi na marehemu nyumba moja baada ya mume wa marehemu ambaye ni Mwenyekiti wa mtaa wa National housing Manispaa ya Bukoba, David Dominick kumchukua na kuishi naye kama mwanafamilia akifanya shughuli za ujenzi akishirikiana na mwenyekiti tangu Novemba, 2022.

Tukio la mauji lilitokea Februari 13, 2023 majira ya saa 12:00 jioni ambapo mtuhumiwa alimpiga marehemu kwa kutumia silaha butu kichwani upande wa kushoto na kumsababishia jeraha kubwa lililopelekea kuvuja damu iliyomsababisha umauti papo hapo na kisha kumbaka na baada ya kutekeleza tukio hilo aliondoka na kuelekea kusikojulikana hadi alipojitokeza hadharani juzi Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live