Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nikki wa Pili kueleza vipaumbele vyake mwezi ujao

NIKI 2.jpeg Nikki wa Pili kueleza vipaumbele vyake mwezi ujao

Tue, 22 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Nickson ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa Mkoa.

Amesema kwasasa anajikita kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa aliyoelekeza ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanatatua kero za wananchi, kuongeza kiwango cha mapato na kushughulikia migogoro ya ardhi.

" Tupo kwa ajili ya kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lengo ni kuhakikisha tunaleta maendeleo kwa wananchi" amesema

Nickson pia ameeleza kuwa ataendelea kujifunza kwa haraka kutoka kwa Viongozi wengine na wakazi wa Mkoa wa Pwani ili kufikia malengo ya kimaendeleo katika Wilaya ya Kisarawe huku akiahidi kuendeleza mchango wake kwenye Tasnia ya sanaa.

Chanzo: ippmedia.com