Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mbeya na kuongeza kuwa ni miradi mbalimbali amepewa kuisimamia, hivyo itakuwa ni utovu wa nidhamu kuukimbia Ukuu wa Mkoa na kukimbilia Ubunge, huku akiacha miradi hiyo bado haijakamilika.
"Itakuwa ni utovu wa nidhamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kutokusikiliza la Mkuu ili nije kuvunjika guu, hapa Mbeya kuna mambo mengi yanafanyika na yanahitaji usimamizi wa karibu sana, tumepata vituo vya afya si chini ya 16 na juzi tumeongezewa Mil 500 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Igawilo sasa nitakapoondoka kugombea Ubunge, itakuwa ni utovu wa nidhamu sababu miradi isipokamilika nina cha kujibu hata kufungwa" amesema RC Chalamila.
Aidha Chalamila ameongeza kuwa, "Ni hekima na busara na itakuwa ni utoto wa kupindukia kama leo hii nitakwenda kuchukua fomu kugombea nikashinda kwenye kura za maoni, halafu huku Mwenyekiti wangu wa Chama cha Mapinduzi nimekwishamkwaza kwa kuwaacha Watanzania wake wakilia na kuhangaika".