Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni simanzi! ndugu wakiaga miili 16 Rombo

Mii Pic Ni simanzi! ndugu wakiaga miili 16 Rombo

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: mwanachidigital

Ndugu, jamaa na marafiki waliofika kuaga miili ya wapendwa wao katika viwanja vya Hospitali ya Huruma iliyopo Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, wameshindwa kujizuia na baadhi kuzimia baada ya kuona miili ya ndugu Yao ikiwa kwenye majeneza.

Ajali hiyo ilitokea Februari 4, katika eneo la Magira Gereza, Kata ya Magira Gereza, wilayani Korogwe, barabara ya Segera - Buiko na kusababisha vifo vya watu 21 mpaka sasa.

Ndugu hao pamoja na majirani walikuwa wakisindikiza mwili wa ndugu yao, Athanas Mrema (59) aliyefariki dunia Februari Mosi, kutokea jijini Dar es Salaam kuja mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko ndipo walipata ajali hiyo.

Katika mazishi ambayo yanafanyika leo, ipo familia moja ambayo inazika watu watano kwa wakati mmoja, familia nyingine wawili pamoja na wengine ambao wanazikwa mwili mmoja mmoja.

Katika viwanja hivi ipo miili 12 ambayo inaagwa leo kwa ajili ya maziko ambayo yanafanyika katika familia iliyopoteza watu 14 katika ajali hiyo.

Chanzo: mwanachidigital