Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngorongoro washauriwa kuwatoza fedha wanaotaka kumuona Faru Fausta

11223 Faru+fausta+pic TanzaniaWeb

Wed, 11 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ngorongoro.Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeshauriwa kuanza kutoza fedha kwa watalii kumuona Faru Fausta (55) ambaye ndiye Faru mzee kuliko wote Afrika.

Wawekezaji hao walitoa wito baada ya kutembelea banda maalum ambalo Faru huyo amehifadhiwa kutokana na uzee wake na kuwa na uoni hafifu hivyo mara kadhaa kunusurika kuliwa na fisi.

Akizungumza leo Julai 11, wakati walipotembelea banda hilo, Mwenyekiti wa chama cha Umoja wa wamiliki wa kampuni za Utalii nchini (TATO) Willy Chambulo amesema faru huyo anaweza kuiingizia mamlaka hiyo fedha nyingi za kigeni kama akitumiwa vizuri.

"Kuna watalii watapenda kuja hapa kumuona huyu faru kwani ana sifa za kipekee hivyo mnaweza kuweka tozo maalum kuja hapa kumuona," alisema

Soma Zaidi:

Chakula cha Faru Fausta kuandaliwa nchini.

Sababu za Faru Fausta kutumia Sh760 milioni kwa mwaka zatajwa

Mkurugenzi wa kampuni ya kitalii ya Sunny Adventure, Ayoub Seleman amesema Faru huyo anapaswa kuingiza fedha na ni ishara nzuri ya uhifadhi.

Akizungumza baada ya maombi haya, Naibu Mhifadhi Mkuu wa NCCAA Asangye Bangu amesema watafanyia kazi ushauri wa wawekezaji hao.

"Ni kweli ni gharama kubwa kumuhifadhi huyu Faru hapa na ni kweli ana umuhimu mkubwa katika uhifadhi," amesema.

Hata hivyo amesema taratibu za kuendelea kuboresha makazi ya Faru huyo zinaendelea.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz