Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugulile alia ubovu wa vivuko kigamboni

Kigamboni Data Ndugulile alia ubovu wa vivuko kigamboni

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kigamboni, Dkt Faustine Ndugulile amewataka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuboresha huduma za vivuko vya Kigamboni kwa kuvifanyia matengenezo ya mara kwa mara.

Dkt Ndugulile alifika Feri, Kigamboni baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu ubovu wa vivuko.

"Nimekuja hapa pamoja na viongozi wa Wilaya na viongozi wengine wa TEMESA kuangalia changamoto hii".

Dkt Ndugulile alikuta kivuko cha MV Kazi kikiwa kimesimama kikifanyiwa matengenezo.

Dkt Ndugulile amewataka TEMESA kuhakikisha kwamba wanafanya ukarabati wa vyombo hivi kwa haraka na kwa muda stahiki.

"Ninawasihi sana Wizara ya Ujenzi na TEMESA kuhakikisha vivuko hivi mnavifanyia ukarabati mkubwa na kwa wakati ili wananchi wa Kigamboni wanaotegemea kwenda mjini kwa shughuli za kikazi na kwa ajili ya kupata mahitaji yao wasiathirike. malalamiko kwa wananchi ni makubwa kwa sasa".

Aidha, kutokana na wingi wa idadi kubwa ya watu na magari wanaotumia huduma ya kivuko, amewataka TEMESA na Wizara ya Ujenzi kuangalia uwezekano wa kuongeza pantoni jingine la nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live