Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu wawili wafariki dunia wakivua samaki Lindi

Lindi Wawili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Pili Mande

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ndugu wawili wa familia moja wamefariki dunia kwa kuzama kwenye Bahari ya Hindi katika pwani ya Shuka mkoani Lindi, baada ya kwenda kuvua samaki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Pili Mande amesema hayo leo Alhamisi Oktoba 12, 2023, wakati akizungumza na Mwananchi Digital ofisini kwake.

Kamanda Mande amesema kuwa watu hao walikuwa wamekwenda kuvua tangu Oktoba 10 na hawakurudi hadi jana (jumatano) miili yao ilipokutwa ufukweni mwa pwani ya Shuka katika Kijiji cha Hingawali.

Kamanda Mande amewataja marehemu hao kuwa ni Twaha Hamis (30) pamoja na Hassan Hamis (35) wote wakazi wa Kijiji cha Hingawali mkoani humo.

"Jana nimepokea taarifa ya kukutwa kwa miili ya watu wawili pwani ya Shuka huko, Kijiji cha Hingawali, Halmashauri ya Mtama na miili hiyo ni ya familia moja na walikwenda kuvua tangu tarehe 10 na walivyoondoka hawakurudi na jana ndio miili yao imeonekana pwani ya Shuka," amesema Pili Mande.

Daktari wa Zahanati ya Mtegu katika kijiji cha Hingawali, Emmanuel Ernest amekiri kupokea miili hiyo na ilifanyiwa uchunguzi, kubaini vifo hivyo.

"Nimepokea miili ya familia moja jana hapa zahanati na nikafanyia uchunguzi ili kubaini vifo vyao, ni kweli hivi vifo vimetokana na kuzama kwenye maji," amesema Dk Ernest.

Baadhi ya wavuvi ambao wanavua katika eneo hilo la Hingawali wamesikitishwa kutokea kwa Vifo hivyo vya familia moja.

"Tumeumia kuwapoteza wenzetu, tulikuwa tunafanya nao kazi hii ya kuvua, kwa kweli ni maumivu makubwa kuwapaoteza ndugu wa familia moja kwa pamoja kwa kweli inauma, lakini hatuna jinsi kabisa," amesemammoja wa wavuvi Bakari Juma.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi limetoa wito kwa wavuvi kuwa makini pindi wanapokwenda kuvua ili kuepuka majanga mbalimbali ikiwemo vifo.

Chanzo: Mwanaspoti