Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu watano waliopoteza maisha wakimuaga Magufuli kuzikwa kesho

Familia Ndugu watano waliopoteza maisha wakimuaga Magufuli kuzikwa kesho

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Ndugu hao wa familia ya Daudi Mtuwa; Susan Mtuwa na watoto wake wawili Nathan (6) na Natalia (5) pamoja na watoto wengine wawili Cris (11) na Michelle (8) wa shemeji zake Susan walifariki dunia katika shughuli hiyo iliyofanyika Jumapili Machi 21, 2021.

Gerald Mtuwa mmoja wa wanafamilia hiyo, amesema kuwa mazishi hayo yatafanyika nyumbani kwao Kimara kuanzia kuanzia saa 4 asubuhi.

“Tunatarajia kuwazika hapa nyumbani baada ya kupata kibali kwa sababu kuna eneo kubwa. Kesho miili itawasili na kulala hapa nyumbani kesho tutaizika,” amesema Mtuwa akibainisha kuwa dada wa kazi hajapatikana wanaendelea kumtafuta.

Chanzo: ippmedia.com