Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu waomba mashine kumnasua aliyekwama mgodini - VIDEO

Wed, 11 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Misungwi. Jitihada za kumnasua, Keo Werema katika machimbo ya dhahabu ya Shilalo Inonelwa wilayani Misungwi mkoani Mwanza hazijazaa matunda  kutokana na vifaa vinavyotumika kuwa duni.

Juzi mchana kifusi kiliwafunika watu 10 wakati wakiendelea na uchimbaji na wanane kuokolewa huku mmoja, Ndaki Juma akifariki.

Matiko Chacha mjomba wa Werema ameiomba Serikali kupeleka mashine maalum ili kuweza kumtoa ndugu yao kutokana na zana wanazotumia kuwa duni.

Zoezi hilo linafanywa na mafundi wa mgodi huo kwa kutumia sululu, miti, moko na nyundo.

“Tunaomba serikali ituongezee nguvu, labda ikija mashine kama skaveta kubwa inaweza kuwa kazi rahisi lakini kwa sasa hali ilivyo ni ngumu kulingana na vifaa duni vinavyotumika,” amesema.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza,  Jumanne Muliro amesema kwamba tukio hilo lilitokea katika duara namba 47 G mali ya Petro Charles na duara namba 50 mali ya Deogratias Lushanga na kulikuwa na wachimbaji 10 waliofunikwa na udongo na kuziba njia ya kutoka.

Pia Soma

Advertisement
 “Wengine waliojeruhiwa ni John Katwale, Mwita George, Masanja Charels, Abdala Abdul, Bengwe Clement, Songa Charels, Emmanuel Mathias, Mangera Meki,” amesema.

Amesema majeruhi wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa matibabu.

Shuhuda aliyekuwa ndani ya duara namba 50 G,  Charles Nchagu ameileza Mwananchi kwamba alitoka nje ya duara kufuata maji wakati akirudi alikutana na wenzake wakikimbia kutoka nje kati ya hao wawili walibaki ndani.

Diwani wa Shilalo,  Maila Maguha amesema jitihada bado zinaendelea licha ya kuonekana kuwa ngumu kulingana vifaa vinavyotumika.

> VIDEO: Mmoja afariki kwa kuangukiwa na kifusi kwenye machimbo

Chanzo: mwananchi.co.tz