Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu wafukua mwili wakazike kwao

Screenshot 2021 12 10 At 13.14.57 660x400.png Ndugu wafukua mwili wakazike kwao

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: millardayo.com

Siku chache baada ya Polisi Mkoani Njombe kutangaza kupatikana kwa baadhi ya viungo vya mwili wa Mfanyabiashara wa vitunguu Mkazi wa Morogoro, Ndugu wa Mfanyabiashara huyo wamefika Njombe na kulazimika kufukua mwili wa Ndugu yao na kuusafirisha kwenda kuuzika nyumbani kwao.

Mfanyibiashara huyo ambaye ametambulika kwa jina la Jackson Charles ambaye ni mkazi wa Kilosa Mkoani Morogoro, alipotea tangu October 22,2021 Wilayani Wanging’ombe na baadaye baadhi ya viungo vya mwili wake vilipatikana katika msitu wa ngaramaro kijiji cha Mtapa Wilayani humo.

Uongozi wa Kata ya Kidugala Wilaya ya Wanging’ombe ambako Marehemu alikuwa anafanyia biashara umesema mwili wa Mfanyabiashara huyo ulikutwa msituni ukiwa umeharibika na baaadhi ya viungo vikiwa havipo na ndipo Serikali ikachukua jukumu la kuuzika hapohapo msituni December 05,2021 kutokana na mwili kuharibika, Mtu mmoja anashikiliwa kutokana na tukio hilo.

Chanzo: millardayo.com