Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugai acharuka Dodoma kufanya vibaya la saba

Fri, 14 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai ameitaka idara ya elimu mkoani Dodoma kujitafakari ikibidi watu waachie madaraka kutokana na mkoa huo kufanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba.

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 14, 2018 Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa mkoani hapa amedai kuporomoka kwa elimu Dodoma chanzo ni idara hiyo.

Katika matokeo ya darasa la saba 2018, Dodoma imeshika nafasi ya 23 kati ya mikoa 26  ikipanda nafasi moja kutoka 24 mwaka 2017 huku halmashauri ya Chemba mkoani humo ikiburuta mkia kati ya halmashauri zote 186 nchini.

Akizungumza katika kikao cha wadau, Ndugai amesema chanzo cha kufanya vibaya ni wakuu wa idara ya elimu.

"Hapa ndiyo tatizo, haiwezekani tukaendelea kuburuta mkia. Yakija matokeo haya mwakani tutawaachia kikao chenu tuondoke," amesema Ndugai.

Spika ameitaja idara ya ukaguzi kuwa inafanya kazi kama miungu watu na inakwamisha juhudi za watu katika ujenzi wa shule.

Amesema wakaguzi wameweka masharti ambayo utekelezaji wake huchukua muda mrefu na kuwakatisha tamaa wazazi kuwasaidia watoto wao.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz