Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndoto ya ofisa elimu Dar matokeo darasa la saba

76681 Mkoa+pic

Sun, 22 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Takribani wiki moja tangu wanafunzi  947,221 kutoka shule 17,051 za Tanzania bara kufanya mtihani wa darasa la saba, ofisa elimu mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hamis Lissu amesema mkoa huo utashika nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani huo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 21, 2019 katika mkutano uliowakutanisha walimu wa shule binafsi na Serikali za mkoa huo pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ulioambatana na utoaji wa zawadi kwa shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa pamoja na walimu na wanafunzi

Amesema Mkoa huo umeshika nasafi ya kwanza katika matokeo hayo kwa miaka miwili mfululizo (2017 na 2018).

“Mimi nina imani katika mitihani iliyofanyika mwaka huu tayari tumefanya vizuri kwa sababu maandalizi tuliyofanya ni makubwa na tutaendelea kubaki katika nafasi hiyo,” amesema.

Katika michezo, amesema kwa  mitatu mfululizo wamekuwa mabingwa kitaifa katika mashindano ya Umiseta na Umitashumta.

“Ushindi tulioupata katika michezo hii umechangiwa na wakurugenzi wa Wilaya tatu zikiwemo Ilala, Kigamboni na Kinondoni,” amesema.

Pia Soma

Advertisement

 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanaendelea kufanya vizuri katika mitihani na darasani.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz