Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndoto ya Chato kuwa mkoa yayeyuka

Rc Shigellaw RC Shigella

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella amewataka viongozi Mkoani humo kuacha upotoshaji juu ya mpango wa kuundwa Mkoa mpya wa Chato badala yake wawe wakweli na kutoa fursa ya taratibu za kisheria kuzingatiwa.

Shigela ameyasema hayo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Mkoa (RCC) na kueleza kwa kuwa baadhi ya wilaya za mikoa jirani hawajaonyesha nia ya kuhamia Chato basi ni vyema mchakato uende taratibu.

Amesema kikwazo kikubwa kilicho onekana ni baadhi ya Wilaya ikiwemo Biharamulo, Nyakanazi na Kakonko ambao waliombwa kuunda mkoa mpya wa Chato wameonyesha hawapo tayari kuunda mkoa mpya.

“Tamisemi walipoandika barua, kwamba tumepokea maoni ya kupata mkoa mpya, wakarudishiwa kwamba sisi hatupo tayari kwa maeneo yetu kuanzisha mkoa mpya kwa mantiki hiyo maana yake yale maombi yetu yamekataliwa.” Shigella.

RC.Shigella ametolea mfano mkoa wa Tanga wenye halmashauri 11, majimbo 12, tarafa 37 na kata 245 ilhali Geita ikiwa na halmashauri sita, majimbo saba na kata 125 hali inayoonyesha hakuna haraka ya kuunda mkoa mpya.

“Ninachotaka kuwaambia viongozi wenzangu, tusijenge matumaini ambayo kama muda wake haujafika, lazima wananchi wetu waelewe kwamba hili suala muda wake haujafika.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live