Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndikilo: Fedha za Tasaf zinapunguza umaskini

Fe1c8e4c136f6a76b6987fd76922fd49 Ndikilo: Fedha za Tasaf zinapunguza umaskini

Thu, 22 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amesema fedha zinazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) zinatekeleza azma ya serikali kupunguza umaskini kwa wananchi.

Aliyasema hayo mjini Kibaha wakati akizungumza na maofisa na madiwani mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji wa Kibaha katika kikao kazi kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Tasaf.

Alisema tangu serikali ilipoanza kutoa fedha kwa kaya maskini, imepunguza umaskini kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa huyo, kaya nyingi zilizolengwa na kufikiwa zimeanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi ikiwamo ya kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara na utengenezaji na bidhaa mbalimbali za kijasiriamali.

"Tumeambiwa kaya zilizo kwenye mpango ambazo zilikuwa kwenye umaskini, zimepunguza umaskini na kufikia zaidi ya asilimia 10 na hii inaonesha jinsi gani mpango huu ulivyokuwa na manufaa makubwa kwa walengwa," alisema Ndikilo.

Alisema kutokana na mafanikio hayo, wataalamu na wahusika wa utambuzi wa kaya maskini wafanye utambuzi kwa usahihi, uwazi, na uwajibikaji ili wasiingize watu wasiohusika ili kuondoa malalamiko ya baadhi ya kaya kuwa hawajaingizwa kwenye mpango huo.

"Mpango huu umekuwa na manufaa makubwa kwani umesaidia watoto kupelekwa kliniki kama moja ya sharti la kupewa fedha hizo, watoto wenye umri wa kwenda shule wanapelekwa na kuna sehemu baadhi wanafunzi wamefaulu kujiunga na kidato cha tano kupitia fedha hizo hivyo wataalamu lazima wafanye jambo hili kwa ufanisi," alisema.

Aidha, alisema kaya hizo ziingizie fedha kwa wakati na wale wanaojihuisha na ujenzi nao walipe kwa wakati na kuhamasisha jamii kujiunga na bima ya afya ili kupata matibabu kwa urahisi na kuwapa lishe bora watoto wao.

Naye Lilian Sabaya kutoka Tasaf alisema katika kufanikisha kaya zote maskini zinafikiwa, watabadilisha daftari katika halmashauri zote 184 za Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa Sabaya, sasa Tasaf imezifikia kaya milioni 1.4 zenye watu milioni saba.

Alisema kaya zitakazoongezwa ni 150,000 zikiwemo ambazo hazikuingizwa kwenye mpango kutokana na sababu mbalimbali ambapo wanufaika wa kaya hizo maskini ni pamoja na watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano, wanafunzi wa shule za awali, wajawazito na watu wenye ulemavu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mussa Ndomba, alisema madiwani wana nafasi kubwa kuhakikisha walengwa wanaingizwa kwenye mpango kwani wao ndio wanaoishi na walengwa halisi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz