Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege yaanguka hifadhi ya Serengeti Tanzania, yaua wawili

76855 Pic+ndege

Mon, 23 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Ndege ndogo ya Shirika la Auric Air imepata ajali leo Jumatatu asubuhi Septemba 23, 2019 katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Ajali hiyo imetokea saa 1:30 asubuhi ambapo ilikuwa ikiruka kutoka Serengeti kwenda Arusha baada ya kushusha watalii.

Katika ajali hiyo, rubani na abiria mmoja wamefariki dunia.

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete akizungumza na Mwananchi amethibitisha kutokea ajali hiyo.

"Tunatoa taarifa zaidi baadaye kwani sasa kazi inayoendelea ni kuokoa vitu na kuhifadhi miili," amesema.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz