Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege yaanguka Tabora, rubani na mhudumu wafariki

69763 Ndege+pic

Sun, 4 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Watu wawili raia wa Afrika Kusini wamefariki dunia baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika kijiji cha Igugwa wilayani Sikonge Mkoa wa Tabora jana Jumamosi Agosti 3, 2019.

 

Taarifa iliyotolewa na sekta ya mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inaeleza kuwa

ndege hiyo yenye usajili  ZU-TAF aina ya SLG4 ilikuwa  ikiruka kutoka kiwanja cha ndege cha Tabora kuelekea kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Lilongwe, Malawi.

 

Inaeleza kuwa chanzo cha ajali  hiyo ni hitilafi ya injini, rubani alitoa taarifa katika kituo cha kuongozea ndege jijini Dar es Salaam na mara baada ya taarifa hiyo ndege hiyo ilipoteza  mawasiliano na kuanguka.

Pia Soma

 

Miili ya watu hao, Desmond Roy Werner (rubani) na Werner Froneman (mhudumu) imehifadhiwa katika Hospitali ya Kitete,  Tabora.

Chanzo: mwananchi.co.tz