Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege waharibifu waliovamia wilaya 22 kudhibitiwa

Cea5f9546b0ecbcf871c621a56fb57a7.jpeg Ndege waharibifu waliovamia wilaya 22 kudhibitiwa

Fri, 14 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI imesema inaendelea na udhibiti wa ndege waharibifu aina ya kweleakwelea waliovamia mashamba katika wilaya 22 zilizopo kwenye mikoa 12 nchini.

Kazi ya kudhibiti ilianza Novemba 17 , 2020 na bado inaendelea.

Aidha imesema kazi ya kudhibiti ndege hao inaendelea pia katika maeneo mapya yaliyoripotiwa katika Mkoa wa Tabora na Simiyu na maeneo ambako yalishadhibitiwa lakini makundi mapya ya kweleakwelea yameanza kujitokeza Wilaya ya Mbarali (Mbeya), Babati (Manyara) na Kishapu (Shinyanga).

Mikoa ambayo imevamiwa na wilaya zake katika mabano ni Kilimanjaro(Mwanga, Moshi), Arusha (Wilaya ya Meru), Manyara (Simanjiro na Babati), Dodoma (Chamwino, Bahi, Kondoa, Dodoma Jiji), Singida (Singida Vijijini, Itigi, Mkalama), Morogoro (Kilosa na Mvomero), Iringa (Iringa Vijijini), Mbeya (Mbarali), Geita (Geita Vijijini), Mwanza (Sengerema na Kwimba) na Shinyanga (Kishapu na Shinyanga Vijijini) na Pwani (Chalinze).

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana kuhusu juhudi za serikali kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao, Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda amelihakikishia taifa kwamba hakuna tishio la nzige wa jangwani baada ya kazi kubwa ya kukabiliana nao kwenye eneo la jumla ya hekta 6,441 nchini.

Kazi hiyo ya kupambana na nzige hao waliovamia wilaya ya nane wakitokea Kenya ilifanyika kuanzia Machi 4, 2021 hadi Aprili 13, 2021 na kwamba mpaka sasa haijabainishwa uwepo wa nzige.

Nzige hao walivamia kwa nyakati tofauti kati ya Januari 14, 2021 na Februari 24, 2020 katika wilaya za Mwanga, Siha, Moshi, Simanjiro, Longido, Monduli, Ngorongoro na Lushoto.

Akizungumzia suala la nzige wekundu nchini, Waziri Mkenda alisema katika msimu wa 2020/2021 wataalamu wa Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Shirika la Kudhibiti Nzige Wekundu la Kati na Kusini mwa Afrika ( IRLCO-CSA) wamefanya uchunguzi katika maeneo yote ya mazalio ya nzige wekundu na kubaini hakuna tishio la uwepo wa nzige hao.

Nzige wekundu huwapo katika mazalio ya asili ya yaliyopo katika Bonde la Mto Malagarasi, Mbuga za IKuu/Katavi , Mbuga za Wembere na Mbuga za Ziwa Rukwa.

Aidha, alisema kuna mazalio madogo kwenye Mbuga ya Bahi.

Pamoja na udhibiti wa nzige na ndege hao pia serikali imeanza kukabiliana na vijeshi vamizi.

"Kisumbufu hiki ni tishio kwa usalama wa chakula, lishe na uchumi wa nchi kutokana na uwezo wake wa kushambulia hadi aina 80 ya mazao yakiwemo mahindi, mtama, uwele, mpunga, shairi, ngano, miwa na kuleta uharibifu wa mazao hadi kufikia asilimia 100 kama hatadhibitiwa mapema na kikamilifu,"alisema.

Profesa Mkenda alisema hatua ilizochukua serikali ni pamoja na kuanza kusambaza mitego ya kunasa nondo wa kiwavijeshi vamizi 289 katika mikoa mbalimbali nchini iliyo na kadhia hiyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz