Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndege iliyoanguka Tabora ilitua bila taarifa, kutozwa faini

69805 Ndege+pic

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Ndege iliyoanguka katika kijiji cha Igungwa wilayani Sikonge na kuua watu wawili ilitua katika uwanja wa ndege wa Tabora bila kutoa taarifa,ambapo wamiliki watatozwa faini.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Agosti 4, 2019 na mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri aliyebainisha kuwa mbali na kutozwa faini kuna taratibu nyingine walielekezwa kuzifuata lakini hakutaka kuziweka wazi.

Amesema huenda baada ya ndege hiyo kupata hitilafu ikiwa angani la Tanzania ilitua uwanjani hapo bila kutoa taarifa.

Ndege hiyo yenye usajili  ZU-TAF aina ya SLG4 ilianguka jana wakati ikiruka kutoka kiwanja cha ndege cha Tabora kuelekea kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Lilongwe, Malawi ikiwa na abiria wawili raia wa Afrika waliopoteza maisha,  Desmond Roy Werner (rubani) na Werner Froneman (mhudumu).

Magiri amesema baada ya taratibu walizopewa kukamilika ilikuwa waendelee na safari yao kuelekea nchini Malawi lakini walishindwa kutokana na kutokuwepo uwanja wa kutua usiku sehemu waliyokuwa wakielekea na kuamua kuondoka jana asubuhi.

Amesema ndege hiyo iliyokuwa ikitokea Uganda kuelekea Malawi wakati ikitoka Tabora, nusu saa baada ya kuruka ilipata tatizo na kuwasiliana na mamlaka husika Dar es Salaam na Tabora na kupewa maelekezo kurejea Tabora.

Habari zinazohusiana na hii

"Inawezekana walikuwa katika jitihada za kurudi Tabora na kupata ajali,” amesema.

Mkuu huyo wa wilaya amesema raia hao wa Afrika Kusini katika Jiji la Durban, walikuwa na utaratibu wa kuelimisha watoto kuhusu mambo ya usalama wa anga na wamefanya kazi hiyo nchi kadhaa zikiwemo Misri na Zimbabwe na kwa Tanzania wamefanya Zanzibar.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz