Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndani ya siku 90 taasisi hizi ziwe zimelipa Tsh. Bilioni 2.3

HOMERA Taasisi zapewa miezi mitatu kulipa deni la mabilioni

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Deni la Sh2.3 bilioni limesababisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kutoa miezi mitatu kwa taasisi zote za Serikali zinazodaiwa na kushindwa kulipa kusitishiwa huduma.

Homera ametoa kauli hiyo leo Jumanne Desemba 7,2021 alipofanya ziara ya kutembelea chanzo cha maji cha Nzovwe kata ya Mwakibete baada ya kupokea taarifa ya kuwapo kwa malimbikizo madeni kutoka  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa,(Mbeya-Uwwas, Mhandisi Gerbalt Kayange.

Mhandisi Kayange amesema kuwa mamlaka inadai Sh2.3 bilioni ikiwa ni malimbikizo ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa kipindi kirefu jambo ambalo linakwamisha kutekeleza miradi mingine na kusogeza huduma kwa wananchi.

Alitaja baadhi ya taasisi zikiwapo za Afya, Jeshi la Polisi, Magereza,na nyinginezo na hivyo kuomba msukumo wa Serikali ili ziweze kulipa fedha hizo.

Wakati huo huo Mhandisi Kayange amesema tayari wamepokea fedha zaidi ya Sh 200 bilioni kwa ajili ya kuanza mradi mkubwa wa maji utakaochukuliwa kwenye chanzo cha mto kiwira Wilaya ya Rungwe ambao utahudumia wakazi 850,000 na kuzalisha lita 125 milioni kwa siku.

Kufuatia kauli hiyo, Homera amesema haikubaliki na kuagiza mamlaka  kuzingatiabkwa muda aliotoa endapo malimbikizo hayo hayalipwa huduma za maji zisizisitiswe

Advertisement ''Ni jambo la kushangaza wananchi wakidaiwa ankara za maji wanakatiwa wakati huo zipo taasisi zimejimbikizia mabilioni ya shilingi sasa nawaagiza mkurugenzi, na mwenyekiti wa Bodi ndani ya miezi mitatu kama hawajalipa wasitishiwe huduma''amesema.

Mwenyekiti wa Bodi, Edna Mwaigomole ameweka  msisitizo kwa Mkuu wa Mkoa na kumueleza tayari kuna barua wamemuandikia ofisini kwake ili kuweza kufanya msukumo Serikalini.

''Mkuu wa Mkoa miradi inakwamba kwani deni hilo ni kubwa sana ambalo lingelipwa haraka fedha zinge elekezwa kwenye miradi mingine ya maji Ili kuwezasha jamii kufikiwa na huduma ya maji safi na salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live