Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nauli Dar-Dom yapanda

97981 Abiria+pic Nauli Dar-Dom yapanda

Thu, 5 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar/mikoani. Wakati Waziri wa Ujenzi, Isack Kamwelwe akiahidi daraja la Kiyegeya barabara ya Morogoro-Dodoma lililosombwa na maji kuanza kutumika kuanzia saa 4:00 usiku wa kuamkia leo, nauli za mabasi zimepanda.

Nauli zilizopanda ni Dar es Salaam kwenda Dodoma kupitia njia ya Iringa.

Daraja hilo lililopo Gairo linalounganisha mikoa ya Dodoma na Morogoro lililosombwa na maji juzi saa 9:00 alasiri kufuatia mvu zinazoendelea.

Juzi kabla ya Serikali kufunga barabara hiyo mamia ya abiria na magari yalikwama eneo hilo huku baadhi wakilazimika kutumia njia mbadala.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini nauli kutoka Dar kwenda Dodoma kupitia Iringa ilikuwa Sh40,000 kutoka Sh22000 kwa basi daraja la kawaida; Sh28,000 hadi Sh45,000 daraja la kati; na Sh50,000 kutoka Sh35,000 daraja la maalumu (VIP) kupitia njia ya Iringa.

Umbali wa kutoka Dar-Iringa hadi Dodoma ni takriban kilomita 760, huku Dar-Moro hadi Dodoma ni kilomita 454.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Waliokuwa wakitoka Morogoro kuelekea Dodoma inadaiwa walikuwa wakitozwa Sh60,000 kutoka kati ya Sh15,000 hadi 30,000, huku Morogoro mjini hadi Gairo ilikuwa 15,000 kutoka Sh5,000.

Pia, gazeti lilishuhudia abiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam wakisubiri mabasi yanayotoka mikoa Singida na Tabora na walilazimika kulipa Sh35,000 badala ya Sh20,000.

Baadhi ya abiria, wapiga debe na wakatishaji tiketi wa kampuni mbalimbali za mabasi kituo cha mabasi cha Ubungo, walisema nauli zimepanda maradufu kufidia.

“Nimekata tiketi ya Sh25,000 kwa basi la daraja la chini ambalo huwa nalipa Sh18000 kwenda Dodoma. Sikuwa na njia mbadala ilinibidi nifanye hivyo,” alisema Iman Zakayo.

Hata hivyo, Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) na kampuni inayojenga reli ya kisasa ya Yap Markez walianza ujenzi wa daraja hilo tangu juzi usiku.

Waziri Kamwelwe aliyetembelea eneo hilo awali aliwaeleza wanahabari kuwa hadi saa 10:00 jana jioni ujenzi ungekuwa umekamilika na magari kuruhusiwa.

Hata hivyo, hadi muda huo lilikuwa bado na Kamwelwe ilipofika saa 12:00 jioni alisema lingetengamaa saa 3:30 usiku na saa 4:00 magari yangeruhusiwa.

Imeandikwa na Bakari Kiango (Dar), Lilian Kasenene (Moro) na Nazael Mkiramweni (Dom)

Chanzo: mwananchi.co.tz