Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Nanenane Simiyu yatanua wigo wa fikira’

4b4c239bfd6207a2d9ea48ef81d60218 ‘Nanenane Simiyu yatanua wigo wa fikira’

Tue, 4 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KUFANYIKA kwa maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi maarufu kama Nanenane kitaifa mkoani Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo kumesaidia kuleta fikra mpya ya ushiriki na maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wakulima nchini.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, ambaye alisema kwao Nanenane si maonesho tu ya kilimo bali ni fursa kubwa ya kilimo biashara yenye tija lukuki na inayolenga kuwajengea uwezo washiriki hasa wakulima, wafugaji na wavuvi.

Mtaka alibainisha juzi alipotembea banda la Benki ya NMB ambapo alisema ni mdau mkubwa wa mafanikio yaliyopatikana na pia imechangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha namna ya taasisi mbalimbali zinavyoshiriki kwenye maonesho hayo na hasa ya mwaka huu.

“Kwetu sisi Nanenane sasa hivi ni zaidi ya maonesho ya kilimo kwani kufanyika kwake hapa kwa miaka mitatu mfululizo kumeyafanya yawe tofauti na hapo awali na kuwa maonesho ambayo mtazamo wake mkubwa ni nyongeza ya thamani kwa washiriki,”alifafanua.

Mkuu wa Mkoa huyo alisema walipoomba kuandaa Nanenane kitaifa walilenga kuwa na maonesho tofauti kabisa na ilivyozoeleka ambayo ndani yake kunakuwa na fursa za kuwajengea uwezo waonyeshaji.

Hii ilitokana na walichokiona na kujifunza walipokwenda Ufaransa, Rwanda na Afrika Kusini kama sehemu ya mkakati wa kujiandaa kuibadirisha Nanenane iwe ya manufaa zaidi kwa wakulima na kilimo pamoja na tija katika maendeleo ya taifa.

“NMB walituelewa na wametusaidia sana kufanikisha kuibadilisha Nanenane ambayo kufanyika kwake Simiyu tangu mwaka 2018 kumeleta mabaliko makubwa sana na hii inaonyeshwa pia na hamasa kubwa walioyonayo wananchi ambao sasa hivi wanafika kwa wingi kwenye viwanja hivi ya maonesho ukilinganisha na siku za nyuma,”alisema.

Alisema walipoanza kutekeleza mpango wa kuwajengea washiriki uwezo na kuwasaidia kuongeza thamani waonyeshaji, NMB ilikuwa peke yake kuusaidia mkoa kufanikisha malengo hayo lakini sasa hivi kila benki na wadau wengine wanafanya hivyo.

Hii ni pamoja na kutoa mafunzo maalumu na elimu kwa makundi mbalimbali wakati wa maonesho na kuwawezesha wale ambao wamewaunga mkono na kuwasaidia kukua kushiriki ili wawe mashuhuda wa mafanikio yanayopatikana.

Akizungumzia mafunzo yanayotolewa na Benki ya NMB kwenye banda lao, kiongozi wa ushiriki wa benki hiyo, ambaye ni Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Sospeter Magese, alisema mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa tangu mwaka 2018 kuwaelimisha wakulima waweze kukua kupitia benki hiyo.

Alisema walianza kwa kutoa mafunzo kwa vyama 20 vya ushirika wa wakulima na idadi hiyo iliongezeka hadi vyama 30 mwaka jana huku mwaka huu wakitarajia kutoa elimu ya fedha na mfunzo ya biashara kwa vyama 40.

Meneja huyo alisema msingi wa mafunzo wanayopewa wakulima ni elimu ya biashara kilimo ili waweze kukifanya kilimo chao kiwe cha kibiashara zaidi na waweze kuwekeza kukiboresha na kukifanya kiwe cha kisasa kwa manufaa zaidi.

Chanzo: habarileo.co.tz