Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nane wafariki ajalini Kigoma

55641 Pic+ajali

Tue, 7 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Uvinza. Watu wanane wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la nyuma na kupinduka mkoani Kigoma.

Akizungumza na Mwananchi jana usiku Ijumaa Mei 3, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 12 :15 jioni katika kijiji cha Mlela wilayani Uvinza mkoani humo.

Alisema gari hiyo iliyokuwa inatokea wilayani Uvinza kwenda Kigoma mjini ilipasuka tairi la nyuma upande wa kushoto na kupinduka.

"Niwaombe wananchi wenye ndugu zao katika ajali hiyo kufika katika hospitali ya mkoa i waweze kutambua miili ya waliofariki dunia,” amesema Ottieno.

Naye Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni, Dk Osmund Dyegula amesema kati ya waliofariki, mmoja alipoteza maisha akiwa anapatiwa matibabu hospitalini hapo.

Amesema walipokea maiti hizo saa 2:00  usiku na kwamba majeruhi wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vyema.



Chanzo: mwananchi.co.tz