Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nane mbaroni wakisafirisha mihadarati

Mihadarati Pic Data Jeshi la Polisi lakamata watu nane waliokuwa wakisafirisha mihadarati

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Jeshi la Polisi mkoani Tanga linawashikilia watu nane kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelekezi kukamilika.

Hayo yalibanishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema hatua ya kukamatwa watuhumiwa hao inatokana na mafanikio ya operesheni na misako.

Misako hiyo imekuwa ikiendeshwa na Jeshi hilo katika maeneo mbalimbali ambapo pia ilifanikiwa kuwakamatwa watuhumiwa wanaojihusisha na biashara za uuzaji wa pombe haramu ya moshi na dawa hizo za kulevya za viwandani.

Alizitaja dawa hizo za kulevya ambazo zimekamatwa kuwa ni kilo 300.08 za mirungi, gramu 4 za Heroine, kilo 87 za bangi na pombe ya moshi (gongo) lita 180.

Wakati huo huo Jeshi hilo limefanikiwa kukamata mali za wizi zikiwamo televisheni 13, vingamuzi mbili, deki ya DVD moja, laptop mbili, simu za mikononi 11 na pikipiki mbili kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi ambao waliibiwa vitu hivyo wafike kituo cha Polisi Chumbageni ili waweze kutambua mali zao.

Kamanda Jongo amesema silaha za kienyeji aina ya magobole 23 yalimatwa katika wilaya za Pangani na Kilindi mkoani humo ambapo watuhumiwa wamekiri kujihusisha na uwindaji haramu.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz